Katika mwendelezo wa kipindi chetu, Maktedis Podium..wiki hii tupo na kijana, George Martine, Ni mkazi wa Sengerema-Mission.
Mjasiliamali kijana, baada ya kushindwa kuendelea na masomo ya ellimu ya juu, alijifunza ufundi stadi kisha kujiajiri..kwa kutazama fursa zilizopo hapa Sengerema, akaamua kuanzisha biashara ya kutengeneza na kuuza MAJENEZA..Sasa anamiliki karakana yake maeneo ya Mission-Sengerema, na ameajiri zaidi ya vijana 15 katika biashara zake, ikiwemo hoteli (restaurant), karakana ya kuchomelea vyuma vya milango na madilisha (welding) na duka la kuuza viambatanisho vya shughuli za mazishi kama, pafyum, sanda n.k